Kuhusu Wifa Cargo
Uzoefu wetu wa kazi
Wifa Cargo ni mabingwa wa usafirishaji wa mizigo Tanzania tukiunganisha Jiji la Dar es Salaam na Mwanza. Tumejikita katika kutatua changamoto sugu zinazowatesa wateja kama vile kuchelewa kwa mizigo, kutokuambiwa ukweli, kutumia madalali wasio waaminifu.
Lengo letu kuu ni kurudisha tabasamu ulilolikosa kwa kukupa huduma iliyonyooka inayozingatia uhakika wa muda na gharama nafuu.
Utaratibu Wetu wa Kazi
Tuna utaratibu wetu maalumu wa usafirishaji mizigo tunayoipokea kutoka kwa wateja hapa Wifa Cargo.
Wasiliana Nasi
Tupigie simu au tuma ujumbe utuelezee mzigo wako na unaenda wapi. Tutakupa bei rafiki ambayo wewe mwenyewe utafurahi.
Upakiaji na Usafirishaji
Tutapokea mizigo yako mara baada ya kukubaliana bei na kuanza hatua za kuupakia kwa umakini mkubwa tayari kwa safari.
Safari hadi kufika
Tutakupa taarifa za mzigo wako tunapoanza safari, ukiwa njiani hadi unapofika. Tunahakikisha unapokea mzigo wake kwa tabasamu na huduma iliyonyooka.
