Tunasafirisha Mizigo Dar - Mwanza

Kila siku tunapokea na kusafirisha mizigo mikubwa na midogo ya wafanya-biashara kwa haraka na kwa bei nafuu.

Tumekuletea Usafiri wa Haraka na Uhakika

Usikubali tena mizigo ichukuliwe na mtu ambaye huna uhakika ana ofisi hapa Dar es salaam au Mwanza. Wafanya biashara wengi wanaoagiza mizigo Dar huwa wanatutumia sana sisi kusafirisha mizigo yao kwa sababu hatuna kona kona.

Sahau kuhusu: Kuchelewa kufika kwa mizigo yako bila sababu za msingi. Unapiga simu hazipokelewi kwa wakati. Bei kubwa isiyoendana na ubora wa huduma unayopata. Uharibifu wa mizigo kutokana na madereva wasio na uzoefu au umakini.

Mhudumu wa Wifa Cargo akipokea oda ya usafirishaji

Aina ya Mizigo Tunayosafirisha

Bidhaa za Biashara

Tunasafirisha bidhaa za duka, nguo, viatu, electronics, na vifaa vya ofisi. Mizigo mingi au michache, tunashughulikia yote.

Vifaa vya Ujenzi

Tunasafirisha cement, chuma, mbao, mabati, na vifaa vingine vya ujenzi. Mizigo mizito au mirefu, tuna gari maalum kwa ajili yako.

Malighafi

Tunasafirisha malighafi za mashambani au viwandani. Malighafi yako itafika ikiwa salama na kwa wakati.

Mizigo Maalum

Kama una mzigo maalum, tuambie. Tunaweza kusafirisha vifaa vya shule, mashine, na vitu vingine vikubwa.

Utofauti wetu na wengine

Hatuna madalali wa kati, sisi ukitupa mzigo tunahakikisa unatoka ofisini kwetu hadi unakufikia na tunahakikisha mzigo wako unafika salama, kwa wakati, na bila wasiwasi. 

Hatuna janja janja  linapokuja suala la kuhudumua wateja ndio maana wateja wetu wengi wanatuamini. Uaminifu ndio kila kitu kwetu.  

  • Tunazingatia muda

  • Bei zetu ni nafuu

  • Usalama 100%

  • Hatuna janja janja

Mizigo iliyo tayari kusafirishwa kwenda Mwanza

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tumekuwa tukipokea maswali haya mara kwa mara hivyo tumekuweke majibu ya maswali hayo hapa. Kama una swali na majibu yake hututajaweka hapa tafadhali wasiliana nasi.  

Ni mikoa gani mnasafirisha mizigo?

Mizigo tunasafrirsha kwenda mwanza pia mizigo ya Dodoma, Singida, Nzega na Shinyaga tunapakia.

Hatusafirishi mikoa mingine. 

Inachukua muda gani mzigo wangu kufika unakokwenda?

Tunazingatia Uhakika wa Muda. Mzigo wako utafika mahali ulipopangwa na kwa wakati uliokubaliwa bila visingizio visivyo na msingi.

Endapo kuna changamoto tutakujulisha mapema

Ofisi zenu zipo sehemu gani?

Hapa Dar es Salaam tunapatikana Ilala karibu na AMANA Hospital mtaa wa Sharif Shamba.

Mwanza tunapatikana Nyamagana mtaa wa Nyakabungo (Maendeleo)

Nitajuaje maendeleo ya mzigo wangu ukiwa njiani?

Hutahitaji kutupigia simu mara kwa mara; tutakupa taarifa za mzigo wako katika kila hatua ya safari mpaka unafika. Pale penye changamoto tutakujulisha mapema.